Pages

Yanga,JKT Ruvu Zaingiza Milioni 66

Mchezo wa ligi kuu ya vodacom kati JKT Ruvu na Yanga iliyochezwa hapo jana (April 21 mwaka huu) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ,imeingiza sh. 66,568,000 kutokana na watazamaji 11,864.

Viingilio katika mechi hiyo namba 106 iliyomalizika kwa Yanga kutoa dozi ya 3-0 kwa wenyeji wao vilikuwa sh.5,000, sh. 8,000 sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,702,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,154,440.68. hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,984,450.40, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,790,670.24 ,Kamati ya Ligi sh. 4,790,670.24,

Mfuko wa Maendeleo ya Mpira Miguu (FDF) sh. 2,395,335.12, chama cha mpira wa miguu cha Pwani (COREFA) sh. 931,519.2 chama cha mpira Dar es salaam (DRFA) sh. 931,519.21.

No comments: