Pages

Wimbo Mpya wa Juma Nature - Fitina. Amekumbushia Alivyokimbizwa na Ndala(Kandambili) Isikilize Hapa

Kitendo cha mtangazaji wa EATV Sam Misago kumtoa nje ya studio Sir Juma Nature weekend iliyopita baada ya kwenda studio kwenye kipindi cha Saturday Night Live akiwa na ndala na kaoshi, hajakichukulia poa staa huyo.
Sir Juma Nature
Licha ya kuwasilisha malalamiko yake kwenye Facebook kutokana na kitendo hicho, Nature hajaishia hapo na sasa amemchana mtangazaji wa kipindi hicho kwenye wimbo mpya wa TMK Halisi, Fitina.
Katika wimbo huo Nature anachana, “Halafu watu wengine sijui wanakuwaga ni mapimbi, eti msanii kaingia studio na ndala na amevaa pensi hakujua anayosema kwenye Facebook na Twitter sijui kisa hela alizopewa na mameneja feki wasiopenda wa Uswazi, mzomeeni huyo, sasa kazi kwake na raia wake.”
Kisikilize kipande hicho hapa chini.

No comments: