
Madee akitumbuiza.

Ney wa Mitego akifanya vitu vyake.

Msanii Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani mashairi yenye mvuto kwa miondoko ya HIPHOP wa mkoani Mwanza maarufu kwa jina la Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la Airtel Yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha

WASANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), wamefunika kwa kutoa burudani ya nguvu kwenye kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel nchini ya Airtel Yatosha na kuwapa raha maelfu ya wapenzi wa muziki huo waliofurika katika viwanja vya wazi vya Furahisha Jijini Mwanza.
Kampeni hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika viwanja hivyo na kushuhudia na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupata ushuhuda wa Airtel yatosha kwa kununua laini za simu za mkononi za Kampuni hiyo na jinsi ya kutumia huduma ya Internet, kuongea kwa kujiunga na kupata dakika nyingi za muda wa maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei nafuu zaidi kwa laini moja tu ya Airtel.
No comments:
Post a Comment