Waziri wa ujenzi Dk. John Magufuli amewaagiza wakandarasi jijini Dar es Salaam waliositisha kuendelea na kazi kufuatia baadhi ya watu kufungua kesi mahakamani kuendelea na kazi ya kujenga barabara hata kama inapita mlangoni bila kubomoa nyumba zao hadi kesi itakapoisha huku akiwataka watu waliogoma kupisha mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kuondoka haraka kabla hawajabomolewa.