Pages

MAN U WAANZA MAZOEZI LEO, CHINI YA KOCHA MPYA DAVIS MOYES

David Moyes
David Moyes ameanza zama mpya Manchester United kwa kuingia uwanjani kuungana na wachezaji kuwafundisha katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington leo.
Kocha huyo mpya wa United aliungana na Msaidizi wake, Steve Round na alikuwa akifanya kazi yeye mwenyewe tofauti na kocha aliyemtangulia, Sir Alex Ferguson, ambaye alifurahia kuwaachia Mike Phelan na Rene Meulensteen kukochi timu.
Mchezaji anayetaka kuondoka, Wayne Rooney, mchezaji mpya, Wilfried Zaha na kocha mchezaji, Ryan Giggs walikuwa miongoni mwa walioshiriki mazozi hayo ya leo.
David Moyes

Zaha alilazimika kufanya vizuri ili kupambana na tetesi kwamba atatolewa kwa mkopo akakusanye uzoefu baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 15 kutoka Crystal Palace.

Na winga huyo kinda wa umri wa miaka 20 kwa kuonyesha kufurahia kuanza kazi United, ameposti picha akiwa na jezi ya mazoezi ya timu hiyo akitweet: "Siku kubwa ya kwanza #MUFC,".

David Moyes
Danny Welbeck na Rio Ferdinand
Danny Welbeck na Rio Ferdinand Wayne Rooney Wayne Rooney alikuwepo leo, ingawa alimaliza vibaya msimu uliopita kwa kutofautiana na Sir Alex Ferguson