Watu takriban 77 wamekufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa kati ya abiria 218 baada ya treni moja ya abiri kuacha njia na kuanguka kaskazini magharibi mwa Hispania.
Mabehewa yote 8 ya treni hiyo iliyokuwa ikitoka Madrid kuelekea Ferrol yameanguka karibu na mji wa Santiago de Compostela.
Taarifa za vyombo vya habari zinasema huenda treni hiyo ilikuwa ikienda kwa mwendo kasi wa mara mbili ya kipimo chake katika eneo lenye kona.
Maafisa mjini humo hawajasema lolote kuhusiana na chanzo cha ajali hiyo huku wachambuzi wa mambo wakisema ni ajali mbaya zaidi ya treni kutokea nchini Hispania katika kipindi cha miaka 40.
Ajali kubwa ya treni kuwahi kutokea nchini humo ilikuwa mwaka 1972 wakati watu 77 walipokufa baada ya treni kuacha njia huko Andalusia eneo la kusini.