Zaidi ya wateja 450,000 wa Kampuni ya Vodacom Tanzania huenda wakakosa fursa ya mawasiliano kutokana na kushindwa kufanya usajili wa kisheria wa namabari zao za simu na hivyo kuilazimu Vodacom
kuzifunga nambari hizo.
Uamuzi huo wa Vodacom umekuja baada ya kumalizika kwa kipindi cha usajili
wa nambari zote za simu za mkononi nchini Julai 10 mwaka huu.
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw. Rene Meza, alisema kuwa ingawa sio jambo
linalofurahisha lakini kama kampuni ni lazima iheshimu na kuzingatia sheria
na kanuni za nchini na hivyo watazifungia nambari hizo.
“Sheria mpya ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya Mwaka
2010, imeainisha kifungu kinachoelekeza Makampuni ya Mawasiliano, namna
ambavyo wateja wake wanatakiwa kusajili namba zao za simu za mikonon
“Tulikuwa na muda wa kutosha kwa wateja wetu kutekeleza wajibu huo wa
kisheria huku tukitoa fursa na njia nyingi zaidi kuwawezesha kusajili
nambari hizo kwa urahisi na wepesi kutumia maduka yetu na pia mawakala wa
M-pesa nchi nzima na kwamba baada ya kumalizika kwa muda wa ukomo wa
kufanya hivyo hatuna budi kuitekeleza sheria kwa vitendo kwa kuzifungia
nambari zote ambazo hazijasajiliwa.”Alisema Meza.
Meza amesema hadi kufikia Julai 10, kampuni yake imebaini kuwa takribani
laini 450,000 hazijasajiliwa na ndizo ambazo zitakazofungwa.
“Tunapenda kuwashukuru wateja wetu kwa muitikio wao wa kujisajili na pia
kwa uvumilivu wao wakati wa utekelezaji wa utaratibu huu wa usajili wa
nambari za simu na uhakiki wa namba na taarifa za wateja ,”alisema.Meza
na kuongeza “Tumekuwa na mafanikio makubwa kutokana na idadi kubwa ya
wateja wetu kujitokeza kusajili nambari zao, hili ni jambo jema kwao na
kwetu sisi, na ni Imani yangu kwamba wale wote waliojisajili wataendelea
kufurahia huduma za mtandao wa Vodacom.”
Kuhakiki usajili wa nambari Mteja wa Vodacom anaweza kupiga *106 #.
Usajili wa namba za simu si chaguo mbali ni suala linaloendana na Sheria
mpya ya EPOCA, ambayo inaelekeza wateja wanaotumia namba za simu ambazo
hazijasajiliwa na ni kosa kwa mteja kutumoia nambari ambayo haijasajiliwa
huku akikabiliwa na adhabau ya ya Shilingi 500,000 au kifungo cha miezi
mitatu au vyote kwa pamoja.
Awali Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa tarehe ya mwisho ya
kusitisha zoezi la usajili wa namba za simu za mikononi kuwa Juni 1, 2013
kabla ya kusogeza mbele hadi Julai 10, 2013 ili kuwapa fursa wateja ambao
hawajakamilisha usajili kufanya hivyo kuepuka kukatiwa mawasiliano.
Mhina Shabani.
Media Executive
0764 61 54 81