
Shekh Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Shekh huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
No comments:
Post a Comment