“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko
tayari tuitwe na watu watusikilize pande zote mbili hasa mlalamikaji na
ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa
akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.