Pages

Mwanablogu(Blogger) Ahukumiwa Miaka 18 Jela kwa “Kuvunja Katiba”

Mahakama Kuu ya Ethiopia
Picha ya kampeni ya Kumwachia huru Eskinder.
Mnamo Mei 1, Mahakama Kuu ya Ethiopia ilitoa hukumu kali kwa mwandishi aliyeshinda tuzo Eskinder Nega, ambaye sasa atatumikia kifungo cha miaka 18 jela. Nega aliwekwa ndani Septemba 2011 na kufunguliwa mashitaka ya “ugaidi” chini ya sheria isiyoeleweka nchini Ethiopia ambayo imekuwa ikitumiwa kuwalenga waandishi wa mtandaoni na wapinzani wa kisiasa. Mashitaka yake na rufani yake vilicheleweshwa mara kwa mara, wakati makundi ya kimataifa ya watetezi wa haki za kibinadamu na uhuru wa kujieleza yaliendelea kuikosoa hukumu na adhabu yake hiyo. EFF, PEN America, ambayo ni Kamati ya Kuwalinda Waandishi, na mashirika mengine yalifanya kampeni ya kumweka huru, na hata jopo la Umoja wa Mataifa liliiona hukumu hiyo kama uvunjifu wa sheria ya kimataifa.

Mohamed Keita wa Kamati hiyo ya Kuwalinda Waandishi katika kuujibu uamuzi huo wa mahakama, “Kushitakiwa kwa Eskinder na waandishi wengine ni dalili za utawala unaoogopa maoni ya raia wake.”
 Eskinder Nega alikwenda Marekani kwa elimu ya juu, akisoma katika Chuo Kikuu cha Marekani kabla hajarudi Ethiopia kufanya kazi ya uandishi. Alianzisha magazeti manne -yote yakikumbana na mkono wa serikali na kufungiwa- na amewahi kufungwa mara kadhaa kwa sababu ya makala zake zilizoonekana kuiudhi serikali. Alinyang'anywa leseni yake ya uandishi wa habari, na hapo ndipo Nega alipoamua kuhamia mtandaoni, akawa mwanablogu anayetumia majukwaa ya mtandaoni kujadili hali ya kisiasa nchini Ethiopia. Wakati waaandishi wengi nchini Ethiopia wamenyamazishwa na wengine kuamua..
 Endelea kusoma Global voices

No comments: