
Mabaki hayo yalikutwa majira ya saa 6:00 mchana, juzikati yakiwa yamesambaratika kutokana na kuoza.
Walioyakuta ni maofisa wa magereza ambao walikuwa katika eneo hilo na wafungwa wakikata miti kwa ajili ya kuni.
Wakizungumza na Amani, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mwanamke huyo inaonekana siku ya kifo chake alikuwa amevaa suruali nyeusi, kilemba cha kitenge chenye madoa mekundu, njano, meusi na meupe pamoja na skafu ya rangi nyeupe na nyeusi.

Mazingira ya kifo cha mwanamke huyo yalionesha utata kwa kuwa hata polisi waliofika eneo la tukio, walikiri kutokuwepo kwa taarifa yoyote ya mtu kupotea na kwamba inawezekana alivamiwa ama alikufa kwa matatizo yake au alikuwa akitoka hospitali ambayo ipo jirani na eneo hilo.
Mabaki ya mwili huo yalichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Chumba cha Maiti cha Nina Marwaha cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.
GPL