Pages

Sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Mohammad (SAW) Zanzibar

Maulidi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Viongozi wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar, alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe
za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana, na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume, (katikati).

Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.

Wanawake mbalimbali waliohudhuria.

Wanafunzi wa Madrasa Munawara Shaurimoyo Wilaya ya Mjini Zanzibar wakisoma Qaswida ya...
Mwaka 1434 el Hijra,wakati wa sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisra mijini Zanzibar.
Ustadh Ali Twalib Mohamed,wa Kibanda Hatari Mjini Zanzibar akisoma Maulid Barzanj Mlango wa kwanza katika kusherehekea kwa kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) kwenye Maulid hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wa tatu kulia) akipokea Marashi
wakati wa kumswalia Mtume (S.A.W) wakati wa sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa kwake katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, iliyotayarishwa na jumuiya hiyo katika sherehe za Maulid hayo jana usiku.

Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria kwenye Maulid hayo