Wananchi wa kijiji cha Kasuro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Rwanda wameendesha operesheni ya kuwaondoa nchini wahamiaji haramu wenye makundi makubwa ya mifugo waliomilikishwa ardhi kinyume cha sheria baada ya serikali kushindwakutekeleza ahadi zake za kuwaondoa takribani miaka kumi iliyopita na kuchochea migogoro ya ardhi na mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.