RAIS Jakaya Kikwete amesema kuna juhudi nyingi zinafanywa kuleta machafuko nchini na kuweka bayana kuwa wapo baadhi ya watu wanaolipwa ili kuchochea machafuko hayo kwa kutumia mgongo wa dini.
Mbali na wanaotumia dini ambao amesema Serikali itawadhibiti, Rais Kikwete pia ameonya kuwa hatakubali uchochezi wa vurugu unaofanyika kwa kupitia vyombo vya habari. Katika hilo, amesisitiza kuwa hatalifungulia gazeti la kila wiki la MwanaHalisi kwa sababu kutaka wanajeshi waasi, siyo uandishi wa habari na haukubaliki.
Rais Kikwete alisema hayo juzi mjini hapa wakati akijibu hoja zilizoibuliwa katika ripoti ya tathmini ya Mpango wa Afrika Kujitathimini Kiutawala Bora (APRM) kwa Tanzania, iliyowasilishwa hapa.
Ripoti hiyo iliwasilishwa kwa viongozi wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika wanaoshiriki APRM na Barrister Muna, ambaye alikuwa kiongozi wa jopo lililofanya tathimini kwa Tanzania.
Katika ripoti hiyo, kulitolewa changamoto kuwa zimeanza kuonekana dalili za mgawanyiko kwa misingi ya dini nchini Tanzania. Changamoto nyingine zilizoainishwa ni madai ya uhuru wa vyombo vya ...
habari kuminywa pamoja na masuala ya haki za binadamu.
“Kwa Tanzania ukabila siyo tatizo, lakini basi kama kuna tatizo linalotishia sasa ni udini. Hii ni tasnia inayolipa fedha nyingi sasa, kuna watu wanalipwa fedha nyingi sana katika suala hili.
“Kuna juhudi nyingi zinafanywa kutumia dini kuleta machafuko nchini. Maana unakutana na watu wanakuuliza kwa nini Tanzania mmekuwa na amani kwa miaka mingi hivi? Yaani wanatamani muingie katika machafuko,” alisema Rais Kikwete.
Alisema anaona dalili kwamba wapo watu wanaotaka kutumia dini kuleta machafuko nchini, lakini akabainisha kuwa Serikali itafanya kila iwezalo kuchukua hatua za kudhibiti wanaotaka kuleta vurugu hizo kwa misingi ya dini.
Alifafanua kuwa uhuru wa kuabudu umetolewa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, lakini uhuru wa kutukana dini nyingine, haukubaliki na hautavumiliwa. Alionya katika kukabiliana na chokochoko za kidini, viongozi wa dini hawana budi kukutana mara kwa mara na kuzungumza ili kuondoa tofauti zao. Uhuru wa habari Rais Kikwete alisema Serikali itaendelea kutoa uhuru kwa vyombo vya habari, lakini haitavumilia uandishi wa habari wenye kuleta chuki na kuwa chanzo cha machafuko nchini.
“Ndiyo, kuna gazeti moja tumelifungia na wapo wanaotaka tuliondolee adhabu, tumesema hapana. Kutaka jeshi liasi, huu si uandishi wa habari, haikubaliki,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema Serikali yake imetoa uhuru mwingi kwa vyombo vya habari nchini kufanya kazi zake na hali hiyo imesababisha baadhi ya vyombo hivyo kumuandika hata yeye Rais mambo mengi.
“Siyo kweli kuwa vyombo vya habari nchini Tanzania haviko huru. Viko huru sana tena wakati huu, kiasi kwamba vimeweza kumshutumu Rais. Wanaandika kuwa rais anasafiri sana kwenda Ulaya,” alisema Rais.
Alisema Tanzania imetoka mbali katika masuala ya vyombo vya habari ikiwa na magazeti mawili tu na redio moja, lakini sasa yapo magazeti 706 yanayochapishwa kila siku, kwa wiki, na kwa mwezi.
Alisema pia idadi ya vituo vya redio imeongezeka kufikia 85, vikiwamo viwili vya Serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati vituo vya televisheni vimefikia 26, vikiwamo viwili vya Serikali.
“Kwa hiyo, kuna mabadiliko makubwa katika vyombo vya habari na uhuru wake pia, kiasi kwamba wakati mwingine yaandikwa mambo yasiyo ya kweli.
“Wenzangu katika Serikali na Chama wananiuliza nini hiki? Wananiuliza umeona walivyokuandika jana. Nawaambia siyo kweli, wanasema sasa kwa nini huchukui hatua,” alifafanua Rais Kikwete.
Alisisitiza Serikali yake kuendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari, lakini akaonya kuwa vile vitakavyokuwa chanzo cha uchochezi na kuleta machafuko nchini, havitavumiliwa kamwe.
Muungano Katika ripoti hiyo, jopo la APRM liliimwagia sifa Tanzania kwa kuwa na Muungano wa kupigiwa mfano Afrika na duniani uliodumu kwa miaka 49 sasa. Muna alisema Umoja wa Afrika (AU) hauna budi kujifunza kutokana na Muungano huo wa Tanganyika na Zanzibar, wanapozungumzia kuanzisha Muungano wa Afrika.
Akichangia hoja katika hilo, Rais Kikwete alisisitiza kuwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea sasa, utazaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imara zaidi. Alisema waasisi wa Muungano huo, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amaan Karume, walikuwa viongozi wenye maono na walichukua uamuzi sahihi kuunganisha nchi hizi mbili.
“Yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa Muungano, lakini umepitia katika vipindi mbalimbali ambavyo wakati mwingine ulikuwa unahisi kuwa Muungano huo sasa utakufa.
“Lakini hivi sasa kuna mchakato wa Katiba mpya unaendelea nchini. Tayari maoni mbalimbali mazuri yametolewa hadi sasa. Wapo wanataka Muungano wa nchi tatu, nne, moja. Kwa hiyo maoni ni mengi, lakini nina imani mwishoni tutapata Muungano imara zaidi,” alisema Rais Kikwete.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana Aprili 26, 1964 chini ya Mwalimu Nyerere na Karume, kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwakani, Muungano huo wa aina yake Afrika na duniani, licha ya changamoto zake utatimiza miaka 50.
Rushwa Akizungumzia suala la rushwa, alisema Serikali yake tangu iingie madarakani imechukua hatua kadhaa zikiwamo za kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, katika kupambana na rushwa.
Alisema sheria kuhusu rushwa imebadilishwa na pia Takukuru imeimarishwa, na kwamba viongozi wabadhirifu wa mali za umma wamefikishwa kortini. “Viongozi wabadhirifu na wanaotumia madaraka yao vibaya wamefikishwa mahakamani. Wengine walikuwa mawaziri wenzangu katika Serikali iliyopita, wengine walikuwa mawaziri wangu na mabalozi.
“Wapo waliohukumiwa, wapo ambao kesi zao zinaendelea na wapo ambao wameachiwa huru kwa sababu Serikali haikuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani. Lakini juhudi katika eneo hili (za kupambana na rushwa) zitaendelea,” alisema Rais Kikwete.

Kutoka Gazeti la HabariLeo
No comments:
Post a Comment