Pages

Mr Blue Atiririka Kuhusiana na Sakata la Shirika la Nyumba la Taifa NHC

Kabaise,Mr Blue
Mkali wa long time kwenye game la Bongo Fleva Tzee Henry Sammir mwenye a.ka. nyingi tu Mr. Blue ameonyesha kukerwa na uzushi kuwa ametupiwa virago aka vyombo vyake nje katika nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Posta jijini Dar es salaam.
Akitia story na Gossip Cop Soudy Brown katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm leo mchana,Blue ama Kabaiser kama anavyopenda kujiita amesema nyumba hizo za shirika la nyumba la taifa NHC alikuwa akiishi mzee wake ambaye amekutana na sakata hilo ambalo tayari limekwishatafutiwa ufumbuzi lakini watu wamechanganya madawa na kudai ni yeye Blue wakati si kweli.
Blue amechukizwa sana na wasambazaji wa habari hizo ambazo zimedai tayari watu walishaanza kugawana pamba zake ambapo amesema watasubiri sana.

No comments: