Na Kibada Kibada wa Fullshangwe-Katavi
Serikali imepiga marufuku Wakuu wa shule za Sekondari wote nchini kuwarudisha nyumbani wanafunzi kwa kisingizio cha kukosa Ada na michango ya aina yeyote ya aina mbalimbaliwatoto wanaoshindwa kuchangia na kulipa Ada kutokana na ama wazazi kutokawa na uwezo wa kulipia kwa wakati michango hiyo. Agizo hilo limetolwa jana na Naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri wakati wa ziara yake mkoani katavi mara baada ya kutembelea shule ya sekondari ya Nsimbo Mkoani Katavi na kusomewa taarifa kuwa baadhi ya wanafunzi wanashinwa kuendelea na masomo kutokana na kukosa ada na michango mbalimbali inayotolewa mashuleni kutokana na wazazi waokuokuwa na uwezo.
“Ni marufuku kwa mkuu yeyote wa shule kuwrudisha nyumbani watoto kwa sababu ya kukosa ada ikiwamo michango ya madawati kwani kumrudisha nyumbani mtoto ni kumuonea michango hiyo adaiwe mzazi wakati mwanafunzi akiendelea na masomo”alisema Naibu waziri.
Alieleza kuwa michango yote inayotakiwa kukubaliwa shule ni lazima Katibu Tawala wa mkoa husika aione na kuridhia kwenye barua na siyo wakuu wa shule kujiamulia kienyeji hali inayoonesha kuwarudisha nyumbani wato ambao ..
hawana Michango hiyo ikiwemo ya madawati.
“Hivi hiyo michango ya madawati kila mwaka madawati hayo yanaenda wapi kwa kuwa kila mwaka mtoto anapoanza kidato cha kwa anaambiwa aende na madawati sasa yanakwenda wapi kama siyo uzembe wa wahusika yanapoharibika kuyatengeneza na kuyatunzo madawati hayo yapoharibika”alisema.Mwanri.
Katika hatua nyingine akizungumzia suala la madarasa manne ya shule ya sekondari ya Kashaulili iliyoko Halmashauri ya Mji wa Mpanda kujengwa chini ya kiwango na shilingi milioni nane zilizotolewa kwenye akauti bila utaratibukufuatwa ambazo zilikuwa za ujenzi wa shule hiyo zifuatiliwe.
Kutokana na kujengwa madarasa hayo chini ya kiwango amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Emmanuel Kalobelo kwa kusaidia na na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima kufuatilia na kuona fedha zilitolewaje benki na matumizi yake yakoje na wahusika ni watu gani kisha ikidhibitika kwamba walitoa fedha Benki bila utaratibu unaoeleweka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
“Sasa naagiza kuwa iwapo watabainika na kuonekana kweli makosa yalifanyika wahusika wachukuliwe hatua za kisheria”alisema Mwanri kwa sauti ya ukali.
Naibu waziri alilazimika kutoa kauli hiyo kufuatiwa maelezo yaliyotolewa na mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi wilaya ya Mpanda Hasani Segela aliyetaka kufahamu hatima ya madarasa hatima ya madarasa hayo manne ya shule hiyo ya sekondari ya kashaulili ambayo ni ya nguvu za wananchi nkwa kuwa ni shule ya kata na watoto wanasomea hapo katika madarasa hayo abayo yanweza kuleta madhara iwapo lolote likitokea.