Mnyama Kakakuona ambaye ana aminika kwa utabiri akirandaranda kwenye hospital ya mkoa wa Morogoro leo.
Askali Magereza akimuwekea vitu mbali mbali mnyama huyo kwa lengo la kutabiri.
Baada ya kuwekewa vitu hivyo mnyama huyo alikwenda kulamba Jembe kama anavyoonekana Pichani.
Baada ya kulamba Jembea pia alikweda kwenye beseni la maji na kuanza kuyanywa.
LEO asubuhi mnyama anayeaminika kwa utabiri Kakakuona ameibuka ndani ya hospital ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro ambapo baada ya kuwekea vitu mbali mbali alichagua maji na Jembe. Wachunguzi wa mambo walisikika wakisema kwamba utabiri wa mnyama huyo ambaye alichagua Maji na Jembe unaashiriki kwamba mwaka huu kutakuwa na mvua nyingi zitakazo ambatana na mafuriko, pia wachunguzi hao walidai kwamba kwa mnyama huyo kuchagua Jembe ni ishara kwamba mwaka huu wakulima watavuna mazao mengi.
Mnyama huyu amechagua maji kwa kuyanywa na baadae kuyakoroga misiri ya mafuliko hivyo ametabiri mwaka huu mvua zitakuwa nyingi sambamba na mafuliko pia alichagua Jembe akitabiri kwamba mwaka huu utakuwa sio mwaka wa njaa wakulima watalima na kuvuma kwa wingi"alisema mzee mmoj aliyejitambushwa kwa jina la Jonas Mkude.