Pages

"Hot-Pot" Zatumika Kuingizia Visu,Bangi na Simu Magerezani

 Magerezani  
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu pamoja na wajumbe wa kamati yake wakiwauliza maswali mbalimbali Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Segerea lililopo jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala Wafungwa na Mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.
Magerezani
Afisa wa Magereza wa Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, Gibson Mwakibibi akiwaonesha mfuniko wa Hot-Pot (chombo cha kuhifadhia chakula) pamoja na Radio, Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambapo vifaa hivyo hutumika kuficha simu, visu, bangi na vifaa mbalimbali ambavyo ni hatari kwa usalama wa mahabusu na wafungwa. Vifaa hivyo vilikuwa vinaingizwa na mahabusu hao na baadhi ya ndugu wanapopeleka chakula gerezani. Hata hivyo, maafisa magereza kwa hutumia chombo cha kugundulia vifaa mbalimbali (Metal Detector) kinachotumika gerezani hapo kuvikamata.