Pages

ZITTO KABWE AWATAKA WANANCHI WAGOME KUILIPA KODI YA SIMU YA SH. 1000 KWA SABABU ILIPITISHWA KINYEMELA

 kodi ya line ya simu
Sakata la kodi ya line ya simu limeendelea kuwakuna wanasiasa wetu ambao wamekuwa wakifunguka kwa nyakati mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.
Baada ya January Makamba, Zitto Kabwe naye amefunguka na kudai kuwa kodi hiyo ni batili na ilipitishwa kinyemela kwa sababu ilikuwa imeshaondolewa....
Huu ni ujumbe wake aliouweka katika account yake ya facebook:
 kodi ya line ya simu
Baada ya kauli hiyo,Zitto Kabwe aliandamwa na maswali mengi sana toka kwa wananchi wakidai kuwa "Makamba alisema tuwalaumu ninyi maana ninyi wabunge ndo mlibariki kodi hii"
Zitto naye alishindwa kulijibu swali hilo na kuwataka wananchi "wachukue simu zao, wawapigie wabunge wao wawaulize ni kwa nini walipitisha kodi hii"
 January Makamba, Zitto kabwe
"Anasema hiyo kwa sababu wabunge ndio waliopitisha.Wabunge ndio wawakilishi wa wananchi.Jambo likipita bungeni hao ndio wa kwanza kulaumiwa.Yupo sahihi kabisa.Mpigie mbunge wako simu muulize kwa nini alikubali au hakupinga kodi hii"