
Habari kutoka ndani ya klabu ya Manchester UTD ya Uingereza zinasema ya kuwa itamualika mwanariadha mwenye rekodi nzuri Duniani Usain Bolt katika mechi ya heshima kwa beki wa klabu hiyo Rio Ferdinand ambaye anatimiza miaka kumi ndani ya Old Tranford, mtanange huo utapigwa mwezi ujao tarehe 9 ndani ya dimba la Old Tranford ambapo Manchester UTD itakipiga na Klabu ya Seville kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu ya Uingereza na nafasi atakayopangwa bolt katika mechi hiyo itatangazwa na klabu ya Manchester hapo baadae. Bolt alikwishawahi kumuomba aliyekuwa bosi wa Manchester Sir. Alex Ferguson lakini hakuweza kupewa nafasi hiyo, Bolt alisema ataonyesha kitu tofauti katika kusakata kabumbu pamoja na kukimbia na mpira kwa spidi yake ya riadha.

Bolt amepewa nafasi hii ya heshima baada kwa muda mrefu kutamani kucheza japo kwa dakika 10 tu katika klabu ya Manchester UTD.