
Rwakatare akionesha alama ya vidole viwili wakati akipelekwa kizimbani.

Wakili wa Rwakatare, Tundu Lisu (kulia) akimuelekeza jambo Mbuge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati wakijaribu kuandaa mipango ya dhamana.

Wakili Peter Kibatara akiweka mambo sawa kabla ya..
kuanza kumtetea Rwakatare.

Wanachama na mashabiki wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili kabla ya kesi kuanza.

Wakili Nyaronyo Kicheere akimuelekeza jambo Godbless Lema baada ya kesi kuahirishwa, kulia ni Tundu Lisu.

Wanachama wa Chadema wakiwa wametawanyika nje ya mahakama baada ya kesi kumalizika.

Rwakatare akipelekwa rumande baada ya kunyimwa dhamana.

Mke wa Rwakatare akitahayari baada ya mumewe kunyimwa dhamana.
Mkuu wa kitengo cha usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilfred Rwakatare leo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka manne ya ugaidi. Rwakatare amepandishwa kizimbanai sambamba na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ludovick Joseph. Yafuatayo ni baaadhi ya matukio yaliyojili mahakamani hapo. Katika kesi hiyo Rwakatare anatetewa na mawakili watano, Tundu Lisu, Profesa Safari, Nyaronyo Kicheere, Mabere Marando na Peter Kibatara.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL