Kupotea kwa pikipiki yake nje ya nyumba ya ufukweni ya Lulu kunamfanya mpiga picha Cheche kuchanganyikiwa. Itakuwaje kama Cheusi atagundua uhusiano wake na Lulu? Cheche anarundika oungo juu ya uongo. Dafu anaahidi kumsaidia kuitafuta pikipiki -- lakini kwa sababu tu anahisi kwa kufanya hivyo atakuwa karibu zaidi na Lulu.
Wakati huohuo, tangu Nusura alipoolewa na Mzee Kizito, Duma amekuwa hana uelekeo na maisha yake. Kovu anamtambulisha kwa mfanya biashara aitwaye Golden kule kwenye kigrosari cha Tula. Lakini Kovu anapolewa na kumtukana bibi yule, Duma anamgeuka na kumtetea Tula -- kitu kinachomfanya yeye na Tula wagundue kuwa wana mambo yanayofanana.