Taifa lipo katika uwezekano mkubwa wa kuingia tena gizani kutokana na kina cha maji katika bwawa la Mtera lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa kushuka na uzalishaji wa umeme kufanyika kwenye kina cha hatari. Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba(pichani), kina cha juu cha maji katika bwawa hilo kinachotakiwa kuzalisha umeme ni mita za ujazo 698.5. Lakini alisema kufikia jana, kina hicho kilikuwa kimeshuka hadi kufikia mita za ujazo 688.68.
Kutokana na hali hiyo, Mramba alisema kuanzia jana walianza ratiba ya kulifunga bwawa hilo nyakati za asubuhi ili kuruhusu maji kuingia na kuanza uzalishaji nyakati za jioni.
Mramba alitoa taarifa hiyo jana mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyotembelea miradi mbalimbali ya Tanesco, ikiwamo chumba cha udhibiti wa umeme Ubungo jijini Dar es Salaam baada ya wajumbe wa kamati hiyo kutaka kujua hali ya uzalishaji umeme kwa kila kituo.
Mramba alisema kutokana na hali hiyo, wameomba kibali Wizara ya..
Nishati na Madini cha kuzalisha umeme kwenye kina cha mita za ujazo 687.5. Alisema kwa kiasi kikubwa umeme unaotegemewa ni kutoka kwenye mabwawa, kubwa likiwa ni la Mtera, ambalo lipo kwenye hali mbaya na umeme kuzalisha kwenye kina cha hatari. Kwa mujibu wa Mramba, kina cha chini cha uzalishaji wa umeme kwenye bwawa hilo, ni mita za ujazo 690. Alisema matarajio ya uzalishaji kwenye bwawa hilo kuwa kwenye hali ya kawaida ni madogo kutokana na mvua za masika na vuli kutokuwa za uhakika, kwani kwa mwaka jana baada ya misimu kumalizika, kina cha maji kilikuwa mita za ujazo 691.4.
Hata hivyo, wabunge walitaka kujua iwapo nchi itaingia kwenye mgawo kwa siku za karibuni, lakini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema uwezekano ni mdogo kutokana na kuwapo kwa umeme unaozalishwa kwa gesi na mafuta.
Alisema bwawa hilo linakauka kutokana na kupungua kwa maji yanayoingia kutoka kwenye mito mikubwa mitatu, huku Mto Ruaha ukishindwa kuingiza maji kwa muda mrefu kutokana na shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.
Aidha, wabunge hao walitaka kujua uzalishaji wa umeme kwa kila kituo.
Meneja Mwandamizi Mdhibiti wa Mfumo wa Umeme, Christian Msiani, alisema Kidatu mashine tatu zinafanya kazi na kuzalisha umeme wa Gridi ya Taifa megawati 90, Kihansi inayozalisha megawati 20, kwa sasa inazalisha megawati 180 kutokana na kuongezeka kwa maji.
Hata hivyo, hali hiyo tete pia ilizungumzwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ambaye alisema iwapo hali ya uhaba wa mvua itaendelea kama ilivyo, hali ya upatikanaji wa umeme itazidi kuwa ngumu.
Simbachawene ambaye ana dhamana ya Nishati, alisema gesi ya Mtwara ndiyo pekee itakayookoa hali hiyo, kwani umeme mwingi utazalishwa kwa gesi na kuachana na utegemezi wa umeme wa maji.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema umeme unaoingia kwenye Gridi ya Taifa kutokana na maji ni megawati 561, mitambo ya gesi inayofanya kazi ni megawati 340 na ya mafuta megawati 375.4. Alisema umeme unaotakiwa kuingia kwenye Gridi ya Taifa ni megawati 1,438 lakini kwa siku ya jana zilikuwa ni megawati 851.
Aidha, alisema kukatika umeme kwa siku za karibuni kulitokana na kituo cha Kipawa kufanyiwa marekebisho kukiwezesha kuzalisha megawati 150 kutoka 90 za awali, ili kuwawezesha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kupata umeme wa uhakika.
Alisema zaidi ya Sh. bilioni 170 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vitano vya kuzalisha umeme katika maeneo ya Ukonga, Kurasini, Mbagala, Kinyerezi na katikati ya mji.
Maswi alisema kwa takriban miaka 30, hakuna ujenzi wowote wa vituo vipya vya kuzalisha umeme umefanyika na hivyo vilivyopo kuchoka na kuzidiwa kutokana na ongezeko la mahitaji ya umeme.
Mjumbe wa kamati hiyo, Martha Mlata, alilitaka shirika hilo kuwa makini na mikataba watakayoingia katika utekelezaji wa miradi hiyo mipya na kutaka iwe yenye kulenga maslahi ya taifa kwanza.
Mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Richard Ndasa, alisema ipo haja kwa serikali kuangalia uwezekano wa kuruhusu uwekezaji kwenye umeme kwa kuingia ubia au kutafuta mikopo kwenye taasisi mbalimbali katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini.
“Mahitaji ya umeme ni asilimia 80, kinachopatikana ni asilimia 19, bado tupo mbali sana, lazima wapatikane wabia tuzalishe umeme kwa wingi. Ni lazima serikali na Tanesco wajadiliane na kuangalia cha kufanya,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco, Jenerali mstaafu Robert Mboma, alisema shirika hilo limedhamiria kwa dhati kuhakikisha nchi inaondokana na giza.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment