Mtoto Simoni Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la Mahenge katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma amelazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa darasa kwanza kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake. Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya.
Mtoto simon Mlope alikumbwa na ugonjwa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo inasababisha kuvuta pumzi kwa shida.
Mama wa mtoto aitwaye AMINA ALLY anaomba Watanzania mumsaidie fedha za matibabu kulinganan na ushauri wa madaktari kuwa mwanaye anatakiwa kwenda nchini India kutibiwa. Alipata rufaa kutoka hospitali ya Muhimbili mwaka 2006 lakini imeshindikana kwenda India tokea wakati huo kwa kuwa huku familia yake haina uwezo.
Amina anasema anajishughulisha na kazi za ndani ambapo hujipatia ujira wa shilingi 30,000/= kwa mwezi.
Baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la SIMON MLOPE ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.
Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia SIMONI MLOPE atumie simu namba+255 752732290
Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake. Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya.
Mtoto simon Mlope alikumbwa na ugonjwa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo inasababisha kuvuta pumzi kwa shida.
Mama wa mtoto aitwaye AMINA ALLY anaomba Watanzania mumsaidie fedha za matibabu kulinganan na ushauri wa madaktari kuwa mwanaye anatakiwa kwenda nchini India kutibiwa. Alipata rufaa kutoka hospitali ya Muhimbili mwaka 2006 lakini imeshindikana kwenda India tokea wakati huo kwa kuwa huku familia yake haina uwezo.
Amina anasema anajishughulisha na kazi za ndani ambapo hujipatia ujira wa shilingi 30,000/= kwa mwezi.
Baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la SIMON MLOPE ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.
Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia SIMONI MLOPE atumie simu namba