SERIKALI Mkoani Iringa imepiga marufuku uchinjaji na ulaji wa nyama ya nguruwe (kitimoto) baada ya kuibuka upya kwa ugonjwa wa homa ya Nguruwe uliopelekea nguruwe zaidi ya 100 katika Manispaa ya Iringa na Iringa vijijini kufa kwa ugonjwa huo. Ugonjwa huo unatishia maisha ya Nguruwe 36,179 wenye thamani ya shilingi bilioni 5, 426,850,000 kwa upande wa wilaya ya Iringa vijijini pekee huku katika Manispaa ya Iringa nguruwe 2812 wenye thamani ya shilingi milioni 421,800,000 wapo hatarini kukumbwa na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment