Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Suleiman Kova
ADAIWA KUWA NI RAIA WA KENYA, ALIKODIWA.
Na waandishi Wetu,
RAIA wa Kenya, Joshua Mulundi (21) amekamatwa na polisi jijini Dar es Salaam na kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumteka na kufanya jaribio la kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka.Mtuhumiwa huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana alasiri na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya.
Wakili Komanya alidai mahakamani hapo kuwa Mulundi ambaye makazi yake ni
Murang'a nchini Kenya kuwa, mnamo Juni 26, mwaka huu akiwa eneo la
Leaders Club, jijini Dar es Salaam alimteka Dk Ulimboka.
Hata hivyo, kumetokea utata wa jina, umri wake na makazi ya mtuhumiwa
huyo, kwani wakati hati ya mashtaka mahakamani inasema ni Joshua Mulundi
mwenye umri wa miaka 21 na mkazi wa Murang’a nchini Kenya, taarifa ya
Jeshi la Polisi imesema anaitwa..
Joshua Mahindi mwenye miaka 31 na mkazi wa Namanga nchini Kenya.
Joshua Mahindi mwenye miaka 31 na mkazi wa Namanga nchini Kenya.
Katika shtaka la pili, Wakili Komanya alidai kuwa tarehe hiyohiyo
mshtakiwa alifanya jaribio la kumsababishia kifo Dk Ulimboka kwa kumpiga
katika eneo la Msitu wa Pande eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam,
kinyume cha sheria.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo akidai kuwa makosa aliyoshtakiwa nayo siyo sahihi.
Hakimu Mkazi, Agnes Mchome alimwambia kuwa hatakiwi kujibu chochote kwa
kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, isipokuwa
Mahakama Kuu pekee.
Hakimu Mchome aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 5,2012 itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Taarifa ya Polisi
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mshtakiwa huyo anajulikana kwa jina la Joshua Muhindi (31), mkazi wa Namanga nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mshtakiwa huyo anajulikana kwa jina la Joshua Muhindi (31), mkazi wa Namanga nchini Kenya.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP) Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mshtakiwa
huyo alikamatwa Juni 29 mwaka huu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima
lililoko Kawe baada ya taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema raia huyo mwenye kitambulisho cha utaifa namba 29166938
kilichotolewa Oktoba 11, 2010 katika Wilaya ya Nyeri nchini Kenya, pia
anamiliki hati ya dharura ya kusafiria yenye namba 0123431 iliyotolewa
Juni 14, mwaka huu Namanga Kenya.
Kwa mujibu wa Kova, baada ya kuhojiwa na polisi, raia huyo alisema
alikuja nchini Juni 23, mwaka huu kwa ajili ya kufanya tukio lililotokea
Juni 25 mwaka huu na kwamba alijulishwa kuwa yeye na wenzake 12 ndiyo
walipangwa kutekeleza tukio hilo.
Alisema raia huyo na wenzake walikuja nchini kwa ajili ya kumdhuru Dk
Ulimboka, baada ya kukodiwa na mtu ambaye hakumtaja jina ambaye anaamini
ni mtumishi wa Serikali.
“Baada ya kuhojiwa alidai kuwa yeye ndiye aliyehusika kumteka Dk
Ulimboka na wenzake na baada ya utekaji huo wenzake waliondoka,” alisema
Kova na kuongeza:
“Alisema walikuja kutekeleza tukio hilo kwa lengo la kujua ni nani
anayemshawishi Dk Ulimboka na alipelekwa na mwenyeji wake asiyemtambua
hadi katika hoteli moja katikati ya jiji.”
Alisema mtuhumiwa huyo na wenzake 12 wako kwenye kikundi kijulikanacho
kama Gun Star chenye makao yake Iwiru Wilaya ya Thika nchini Kenya na
kwamba kinaongozwa na mtu mmoja ajulikanaye kama Silencer akisaidiwa na
Paft.
Alisema pia, mtuhumiwa huyo alidai kuwa, wamekuwa wakijihusisha na
matumizi ya silaha na kwamba wamekuwa wakifanya matukio mengi ya
kihalifu nchini Kenya.
Alisema baada ya utekaji huo, Juni 29 mwaka huu raia huyo alikwenda
katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko Kawe kwa nia ya kutaka kuonana
na kiongozi wa kanisa hilo Mchungaji Gwajima, lakini hakufanikiwa
badala yake alionana na msaidizi wake ajulikanaye kama Joseph Marwa
Kiriba.
“Alipoonana naye alimweleza kuwa yeye ni mwanachama wa Kikundi cha
‘Umafia’ na kwamba hukodiwa kufanya matukio ya kihalifu Kenya na nje ya
mipaka,” Kamanda Kova alisema.
“Alikwenda katika kanisa hilo kwa ajili ya kufanya toba maana aliona
alifanya kitendo cha kinyama hivyo aliona arudi ili akapate toba,”
alisema.
Alisema jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwatafuta watu wengine waliohusika na utekaji huo.
Katika hatua nyingine, jeshi hilo pia limewakamata watu wanane ambao
wanadaiwa kuhusika na uvamizi wa mashamba katika eneo la Kawe.
Maandamano ya madaktari yazuia
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limepiga marufuku maandamano ya madaktari yaliyopangwa kufanyika Jumatatu ijayo kushinikiza mambo kadhaa ikiwamo kuundwa tume huru ya kuchunguza kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limepiga marufuku maandamano ya madaktari yaliyopangwa kufanyika Jumatatu ijayo kushinikiza mambo kadhaa ikiwamo kuundwa tume huru ya kuchunguza kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleman Kova aliwaambia waandishi wa
habari jana kuwa maandamano hayo hayatafanyika kutokana na sababu
mbalimbali zikiwamo za kiusalama.
Alisema wamesitisha maandamano hayo kwa sababu madai ya madaktari tayari yameshashughulikiwa na Serikali.
“Tumesitisha maandamano kwa sababu tunahofia kunaweza kutokea uvunjifu
wa amani maana Waislamu nao walipanga kuandamana kesho (leo),” alisema
Kova.
Msimamo wa madaktari
Kauli hiyo ya Kova ilitolewa saa chache baada ya kikao cha zaidi ya
madaktari 400 waliokutana katika mkutano wa dharura ulioitishwa na Chama
cha Madaktari (MAT), ambako waliridhia kufanyika kwa maandamano hayo.
Katibu wa (MAT) Dk Rodrick Kabangila alisema katika kikao hicho,
madaktari hao walipokea taarifa ya MAT iliyoeleza hatua zilizochukuliwa
na Serikali dhidi ya wenzao waliofukuzwa.
“Madaktari wamepokea taarifa za wenzao kufanyiwa vitendo vya
unyanyasaji, ikiwamo kufukuzwa katika makazi yao kwa kutumia Polisi wa
Kutuliza Ghasia (FFU), kunyimwa chakula, posho na kuelezea kuwa vitendo
hivyo ni vya unyanyasaji na uonevu dhidi ya taalamu na udaktari
wenyewe,” alisema Dk Kabangila.
Dk Kabangila alisema kuwa, kufuatia hatua hiyo madaktari hao wamepitisha
azimio la kufanya maandamano ya amani ambayo yanatarajia kushirikisha
madaktari zaidi ya 800 hadi 1,000 na kutoa wito kwa wananchi wenye
mapenzi mema na taaluma hiyo, kushiriki wakiwa na vitambaa vyeupe.
Akizungumzia msimamo wa polisi kuyazuia maandamano hayo, Dk Kabangila
alisema uongozi wa madaktari utakutana kujadili tamko hilo la polisi.
“Tumepata barua inayozuia maandamano yetu. Barua hii imetoa sababu
ambazo ni tofauti na sisi tulichoomba. Sisi (MAT) ndio tulioomba
maandamano kwa ajili ya kuonyesha hisia zetu juu ya vitendo
wanavyofanyiwa madaktari,” alisema Dk Kabangila.
Habari hii imeandaliwa na Geofrey Nyang’oro, Nora Damian na James Magai
No comments:
Post a Comment