Pages

Msama on The Hunt For Fake CDs.

www.darslamproductions.blobspot.com
KAMPUNI ya Msama Promotions, imekamata watu watatu wakiwatuhumu kuuza kazi za wasanii kinyume na taratibu.
Akizungumza na Dira ya Mtanzania, Mkurugenzi wa Msama Promotions,  Alex  Msama (pichani),  alisema vijana hao walikamatwa katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
Waliokamatwa katika tuklio hilo ni Malik Sultan, Ally Msangi, Edward Michael na  Sijali Andrew ambao walikuwa na CD feki 322 za wanamuziki mbalimbali na wasanii wengine.  
Msama alisema zoezi la kukamata wezi wa kazi za wasanii linaendelea kwa kufanya uchunguzi katika maeneo sugu ambako hatua inayofuata ni kwa wale wanauza kazi hizo mikononi.
Aidha Msama analishukuru  Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa timu ya vijana wake wanaosaka wezi wa kazi za wasanii.

No comments: