Paroko wa Parokia ya Isimani mkoani Iringa,Padri Angelo (katikati) akiwa katika ibada maalumu ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi, anarudi kwao Italia.
Mh: Wiliam Lukuvi (MB) akijumuika na baadhi ya wananchi wa jimbo la Isimani kwenye ibada maalumu ya kumuaga Padri Angelo.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera na uratibu wa bunge ,Wiliam Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Ismani akimfariji msaidizi paroko wa Parokia ya Isimani Herman Myalla (36) wa Kanisa aliyekuwa amelazwa Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kuvamiwa na majambazi juzi

Kuvamiwa kwa paroko huyo kulimfanya Rais Dkt Jakaya Kikwete kutoa pore kwa paroko huyo kupitia waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa ambako paroko huyo na mwenzake walivamiwa
Paroko huyo aliyevamiwa Novemba 15 mwaka jana ameagwa rasmi jana jumapili hafla iliyoshuhudiwa na waziri Lukuvi pia
Paroko huyo alivamiwa na watu watano ambao hadi sasa kesi hiyo bado ipo mahakamani kufuatia watu hao kukamatwa na polisi baada ya uvamizi huo na ambao walimjeruhiwa vibaya paroko na kumpora zaidi ya sh Milioni 3.8
Kuondoka kwa paroko huyo kumeonyesha kuwaliza waumini wa parokia hiyo ya Isimani wilaya ya Iringa akiwemo mbunge wa jimbo la Ismani waziri Lukuvi kutokana na michango mbali mbali ya kimaendeleo ambayo paroko huyo alipata kuielekeza katika parokio hiyo.