
Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo...
Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.
Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii.
Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.
Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Mama Michelle Obama
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF akiongozana na mama Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack Obama Mama Michelle Obama katika ofisi za WAMA jioni hii
Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wake wa Viongozi wakati alipowasili katika ofisi za WAMA tayari kwa kumpokea mgeni wake Mama Michelle Obama.