Pages

SPIKA WA BUNGE LA OMAN NA UJUMBE WAKE WAWASILI DODOMA, ASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO BAINA YA BUNGE LA TANZANIA NA BUNGE LA OMAN

OMAN
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Abdulkarim Shah
Kaminisha wa Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Abdulkarim Shah akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
 Job Ndugai
Naibu Spika Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah kwa Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali alipowasili Dodoma jana.
Anne Makinda
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Dodoma ambapo anafanya ziara ya kibunge ikiwa ni pamoja na kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Anne Makinda
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda pamoja na Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali wakisaini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
 Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali
Wakibadilishana mikataba ya Makubaliano.
 Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali

Picha ya Pamoja Ujumbe wa Spika wa Bunge la Oman na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania.
Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali akiwa na ujumbe wa Wabunge toka Oman yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku sita ambapo pamoja na mambo mengine amesaini mkataba wa uanzishwaji wa ushirikiano wa Bunge la Tanzania na Bunge la Oman katika Maswala mbalimbali. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge