Pages

AWAMU YA PILI YA MAJINA YA WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA NA KAMBI ZA JKT WALIZOPANGIWA...TAREHE YA KURIPOTI NI LEO...!!

JESHI LA KUJENGA TAIFA
JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2013 NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KATIKA MAKAMBI YARUVU PWANI, MGAMBO TANGA, MSANGE TABORA, BULOMBORA KIGOMA, MARAMBA TANGA, RWAMKOMA MARA, MLALE RUVUMA NA KANEMBWA KIGOMA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI HAYO TAREHE 24 JUNI 2013 KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI. 
VIJANA HAO WARIPOTI KATIKA MAKAMBI WALIYOPANGIWA KAMA ILIVYOONYESHA KATIKA TOVUTI YA JKT WWW.JKT.GO.TZ. ATAKAYERIPOTI KAMBI AMBAYO HAKUPANGIWA HATAPOKELEWA. VIJANA HAO WALIPOTI WAKIWA NA VYETI VYA LEAVING VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA KWA UTHIBITISHO 

INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA 
VIJANA WATUNZE TIKETI ZAO WALIZOTUMIA KWENDA KATIKA MAKAMBI YA JKT. NAULI ZAO ZITAREJESHWA NA JKT WATAKAPORIPOTI KAMBINI. 

VIJANA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA PILI NI WALE WALIOFAULU KWA DIVISIONI, II NA BAADHI YA DIVISION III MCHEPUO WA SAYANSI. 
VIJANA WA KIDATO CHA SITA 2013 AMBAO MAJINA YAO HAYAKUORODHESHWA KATIKA TOVUTI HIYO, WATAJIUNGA NA JKT AWAMU YA TATU MWEZI SEPTEMBA 2013. 

KWENDA BULOMBORA JKT -KIGOMA
KWENDA KANEMBWA JKT - KIBONDO-KIGOMA
KWENDA MARAMBA JKT - TANGA
KWENDA MGAMBO JKT KABUKU-TANGA
KWENDA MLALE JKT SONGEA -RUVUMA
KWENDA MSANGE JKT -TABORA
KWENDA RUVU JKT - PWANI
KWENDA RWAMKOMA JKT - MUSOMA-MARA

No comments: