Pages

HATIMA YA ROONEY MAN UNITED ITAJULIKANA KESHO BAADA YA KIKAO CHAKE NA MOYES

Wayne Rooney KOCHA David Moyes anajiandaa kukutana na Wayne Rooney na wawakilishi wake kwa mazungumzo kesho, hilo likiwa jukumu lake la kwanza kubwa tangu aanze kazi Manchester United.

Mkataba wa miaka sita wa Mscotland huyo umeanza rasmi leo na atakwenda makao makuu ya klabu, Carrington kutatua sakata la muda mrefu la Rooney kutaka kuondoka.

Moyes anataka Rooney abaki, lakini anafahamu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 25.6 mwaka 2004 anataka kuondoka.
Tingisha: Wayne Rooney alikuwa kwenye tamasha la muziki Glastonbury mwishoni mwa wiki
Wayne Rooney
Chini ya utawala mpya: Moyes anashikilia mustakabali wa Rooney Old Trafford
Inafahamika mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amejenga fikra zake kwamba kubadilisha klabu ni njia nzuri kufufua makali yake kuelekea Fainali za Kombe la Dunia majira yajayo ya joto.

Zaidi itategemea na mazungumzo yake na Moyes ambaye anafanya jitihada za kumbakiza.
Arsenal na Chelsea zote zinamfuatilia na zina ya kumsajili Rooney na ikiwa United itakubali kumuuza watalazimika kumuacha ajiunge na moja ya wapinzani wao katika Ligi Kuu England.