Taasisi ya Human settlement of Tanzania-HUSETA- imewataka wananchi kujitokeza katika maandamano yatakayoanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi ubalozi wa Uingereza kuwasilisha azimio la kuitaka serikali ya Uingereza kutoa tamko hadharani la kutohusika na maovu yanayofanywa na baadhi ya raia wa nchi hiyo dhidi ya taifa la Tanzania ikiwemo kashfa na udhalilishaji kwa viongozi wa Ngazi za juu wa serikali.