Maisha yanakuwa magumu kwa Cheche hasa pale Lulu anapoanza kumsumbua kwa kumhitaji. Inabidi sasa apambane na maswali yenye ukweli kutoka kwa Shoti, kuhusu mazingira ya uhusiano wake na shangingi lile, pamoja na kero kubwa toka kwa rafiki yake Dafu anayeyaingilia maisha yake. Mke wake, Cheusi, naye anapata utulivu wa akili toka kwa muuza urembo wa mitaani.
Mabadiliko makubwa yanatokea kwenye maisha ya Nusura pale anapojitayarisha kuolewa na Mzee Kizito. Mpenzi wake, Duma ni wa mwisho kujua kuhusu ndoa hiyo. Na pale anapofahamu hilo toka kwa Masharubu, baba yake Nusura, kunazuka tatizo kubwa.