Mtoto Mwigulu Matonange (10)ambaye amekatwa mkono wa kushoto na watu wasiojulikana mkoani tabora akiwa na baba yake Gimbishi kwa mwaka huu walemavu wa ngozi(Albino)wamekua wakikatwa mikono ya kushoto, ikiwa ni tofauti na miaka mitatu iliyopita ambapo waliokumbwa na ukatili huo walikatwa mikono ya kulia.
--
BAADA ya kuibuka upya kwa matukio ya kuuawa na kukatwa viungo vya miili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), wanaharakati nchini wameitaka Serikali kuchunguza kwa kina sababu za mauaji hayo, kuimarisha ulinzi hasa katika maeneo wanayoishi watu wa kundi hilo.
Wakati wanaharakati hao wakieleza hayo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mauaji hayo yanatokana na baadhi ya watu kuwa na imani za kishirikina, kwamba wakipata viungo vya watu wenye ulemavu watapata utajiri.
Alisema tayari Serikali imemuagiza Ofisa Maendeleo ya Jamii Rukwa ambao ulikumbwa na mauaji hayo, kukutana na maofisa maendeleo wa wilaya zote za mkoa huo kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, jumla ya albino 72 wameuawa, 34 wamenusurika, wengi wao kwa kukatwa viungo au kuumizwa. Makaburi 15 yamefukuliwa na viungo kuchukuliwa na kumekuwa na majaribio manne ya kufukua makaburi.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea....>>>>>>