Mahakama ya utawala ya Cairo yaliamua kuwa wakuu lazima wachukue hatua kupiga marufuku Youtube nchini na tovuti nyengine yoyote iliyoruhusu filamu hiyo kuoneshwa.
Kesi hiyo ilipelekwa mahakamani na wakili mmoja wa Misri, Hamed Salem, ambaye amewahi kushtaki mashirika mengine ya habari na watu wanaoonekana kuwa wanatusi Uislamu.
Mwezi uliopita mahakama moja ya Misri ilithibitisha hukumu ya kifo kwa Wamisri wasiokuwako mahakamani, kwa kuhusika na filamu hiyo.