Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, Diamond aligongana na mwanamke huyo kwenye Barabara ya Kimweri, Msasani, Dar es Salaam, saa 3 usiku.
Na Makongoro Oging'
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, amepatwa na kile kinachoonekana ni balaa nambari moja tangu apate umaarufu.
Kenyela alisema, askari wa barabarani walichunguza na kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni pikipiki ambapo wakati Diamond anakata kona, alijaribu kuikwepa pikipiki hiyo ndipo akakutana uso kwa uso na Rav4 la mwanamke huyo.
“Baada ya kugongana, gari la Diamond liliendelea kuserereka na kuigonga pikipiki pamoja na aliyekuwa anaiendesha. Hakuna aliyefariki kwenye ajali hiyo, wote walipata maumivu.”
Kwa upande mwingine, ilibainika kuwa Diamond baada ya kupata ajali hiyo, alikwenda Hospitali ya TMJ kwa matibabu baada ya kujihisi amepatwa na maumivu.
Diamond hakupatikana ili kuzungumzia ajali hiyo lakini kwa kumbukumbu, kabla ya kumiliki gari hilo la kifahari aliwahi kumiliki magari mengine mawili, likiwemo lile alilokaa nalo kwa muda mrefu, Toyota Opa lakini hakuwahi kupata ajali ya kiwango hicho.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, amepatwa na kile kinachoonekana ni balaa nambari moja tangu apate umaarufu.
“Baada ya kugongana, gari la Diamond liliendelea kuserereka na kuigonga pikipiki pamoja na aliyekuwa anaiendesha. Hakuna aliyefariki kwenye ajali hiyo, wote walipata maumivu.”
Kwa upande mwingine, ilibainika kuwa Diamond baada ya kupata ajali hiyo, alikwenda Hospitali ya TMJ kwa matibabu baada ya kujihisi amepatwa na maumivu.
Diamond hakupatikana ili kuzungumzia ajali hiyo lakini kwa kumbukumbu, kabla ya kumiliki gari hilo la kifahari aliwahi kumiliki magari mengine mawili, likiwemo lile alilokaa nalo kwa muda mrefu, Toyota Opa lakini hakuwahi kupata ajali ya kiwango hicho.
No comments:
Post a Comment