Pages

Askari Polisi Wazuia Raia Wasipate Elimu ya Ukimwi

DarSlam 
  Katika hali ya isiyo ya kawaida askari polisi zaidi ya watatu waliokuwa katika doria katika maeneo ya kata ya Makorongoni mjini Iringa jana usiku walizuia tamasha la elimu ya UKIMWI lililokuwa likiendelea nje ya vibanda vya UV CCM mjini Iringa
Askari hao ambao walikuwa na silaha walifika eneo hilo na kuwataka waandaaji wa tamasha hilo ambalo tayari lilikuwa limeanza kusitisha tamasha hilo na kuondoka eneo hilo kwa madai kuwa..
hawana kibali cha kufanya shughuli hiyo ya elimu dhidi ya UKIMWI.
Waandaaji hao ambao walikuwa wakielimisha wananchi waliokusanyika katika eneo hilo kuhusu matumizi ya Dume kondom na kuelezwa hali ya maambukizi ya VVU katika mkoa wa Iringa na kuwataka kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo .
Kitendo hicho cha polisi Iringa kuzuia wananchi kupewa elimu ya UKIMWI wananchi waliokuwepo eneo hilo walionyesha kuchukizwa na uamuzi huo na kudai kuwa uamuzi huo ni sawa na kuwataka wananchi wa Iringa kuendelea kufa kwa UKIMWI.
Kwani walisema maeneo kama hayo ni sahihi kupewa elimu ya UKIMWI na kuwa ni vema elimu ya UKIMWI ambayo imekuwa ikihimizwa na Rais Dk Jakaya Kikwete ikaendelezwa badala ya polisi kuwatisha watoa elimu na kutaka kuwafikisha mahabusu .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma alipotafutwa kwa njia ya simu ili kutolea ufafanuzi suala hilo aliahidi kulifanyia kazi zaidi. 
 Na Francis Godwin

No comments: