Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka jana
mchana alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili
ya kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari
kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko
wa ubongo.
Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya
saa ..
8.30 na ndege aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo
kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha
matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela
Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani
ya uwanja huo.
No comments:
Post a Comment