
Habari hii inatokea Nchini Kenya ambapo Msichana mwenye umri wa miaka 14 Mwanaharabu Wamukoya kutoka katika kijiji cha Harambee katika wilaya ya Kakamega amejifungua watoto watatu wote wakiwa ni Wavulana wawili kati yao
wamezaliwa wakiwa na uzito wa 1.5 kilogram na mwingine akiwa na uzito wa Kilogram 1.3.
Nesi wa zamu katika Hospitali hiyo ya Bugoma Bi,Mary Marumbu alisema Watoto hao pamoja na Mama yao wanaendelea vizuri na wakati wowote wanaweza kuluhusiwa kutoka Hospitalini hapo. Mshangao zaidi ni pale ilipokuja kujulikana kwamba Baba Mzazi wa watoto hao watatu waliozaliwa bado ni mtoto mdogo kama alivyo Mama yao kwani Baba yao ana Umri wa Miaka 16 ambae pia bado anasoma, Zaidi aliishukuru sana Serikali kwa kuweza kuondoa garama kwa wajawazito wakiwa wanajifungua na ivyo kuweza kumuwezesha mzazi mwenzie kujifungua pasipo Garama zozote zile.