Pages

WAZEE WANAOISHI NDANI YA KAMBI YA MATESO MOSHI

Joseph Musa,Inyasi Athanas,Joseph Mbole na Ramadhan Kalwinzi
Kutoka kushoto ni Joseph Musa,Inyasi Athanas,Joseph Mbole na Ramadhan Kalwinzi
Hawas ni wazee ambao ni sehemu ya maelfu wazee waliotapakaa kila kona nchini ambao hawana matunzo mazuri. Wazee hawa, wanalelewa kwenye kambi ya wazee wasiojiweza kwenye ya Njoro iliyopo katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maisha ya wazee hawa ni zaidi ya kambi ya mateso.
Kwanza hawapatiwi huduma za afya inavyostahili, 
Pili wanakufa kutokana na lishe duni na (uzee wao).
Tatu wazee hao wanaishi mazingira ya kutisha kutokana na kambi yao kuvamiwa na vibaka mara kwa mara na kuporwa vitu vyao.
Nne, vyumba wanavyoishi hakuna hewa nzuri kutokana na kutokuwa na madirisha yenye kutoa hewa safi, 
Tano, vyoo wanavyotumia kujisaidia viko umbali mrefu kutoka nyumba wanamolala na vimejengwa enzi za utawala wa kikoloni ambapo (wengine tulikuwa bado hatujaiona dunia)
Sita, wazee hawa wakiugua hakuna gari la kuwakimbiza hospitalini na msimamizi wa kituo hicho, hulazimiki kuingia mfukoni mwake kuwanusuru na mauti wazee hao.
Saba, akina mama wanaowahudumia wazee hao, wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya kuambukizwa kutokana na kufanya kazi katika mazingira magumu pasipo kuwa na vitendea kazi maalum.
Mwisho,sera ya wazee iliyotungwa na serikali ipo. Lakini inatia shaka katika utekelezaji wake.
Pamoja tutafakari na kuchukua hatua. Tusipowajali wazee, nasi yaweza kutukuta haya.