Jeshi la polisi mkoani Arusha limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi na viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Soweto ulipotokea mlipuko wa bomu baada ya kukaidi amri ya kutawanyika katika eneo hilo iliyotolewa na jeshi hilo.