
AKIZUNGUMZA JANA NA WAANDISHI JIJINI HAPA MBOWE ALISEMA,WAMEGUNDUA RISASI ZA SMG PAMOJA NA BASTOLA ZILIZOTUMIKA BAADA TU YA BOMU LILE KURUSHWA NA RISASI KUANZA KUPIGWA MFULULIZO KUELEKEA WALIPOKUWA.
AMESEMA KUWA TUKIO HILO WANALICHUKULIA KWA UZITO MKUBWA NA BAADAE WATATOA MAJUMUISHO YA UCHUNGUZI WA TUKIO ZIMA HUKU WAKIONYA KUWA MATUKIO HAYA YANAWEZA KULIPELEKA TAIFA KATIKA MGOGORO MKUBWA AMBAO WAATHIRIKA WAKUBWA MWISHO WA SIKU WANAKUWA NI WANANCHI WA CHINI.
AMEOMBA JESHI LA POLISI IKIWA WANATAKA KUJENGEWA IMANI NA WATANZANIA WAFANYE UCHUNGUZI HURU NA WA HAKI ILI KUBAINI HASA MLIPUAJI ALIKUSUDIA NINI KATIKA TUKIO HILO.
HATA HIVYO MKUU WA JESHI LA POLISI BWANA SAIDI MWEMA AMEWATEUWA MAKAMISHNA WAWILI AKIWEO PAUL CHAGONJA KWENDA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA ILI KUBAINI KADHIA HII.