Pages

Madam Rita na Water Chilambo Wakizindua Bongo Star Search 2013 (Video)

Shindano la kusaka vipaji vya uimbaji muziki la Epiq Bongo Star Search, EBSS, leo limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliofanyika makao makuu ya Zantel umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen a.k.a Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na mmoja wa majaji shindano hilo, Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan pamoja mshindi wa shindano hilo mwaka jana, Walter Chilambo.