Pages

Chelsea Imelamba Mkataba wa Maana na Adidas.

 Uefa Europa League Chelsea Mabingwa wa Uefa Europa League Chelsea wamesaini mkataba mkubwa wa udhamini kuliko yote kwenye historia ya mchezo wa soka . The Blues wamesaini mkataba wa miaka kumi na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya adidas ambao thamani yake ni paundi milioni 300.
Mkataba huu unauzidi mkataba uliokuwa unashikilia rekodi kati ya Manchester United na kampuni ya Nike uliosainiwa mwaka 2000 ambao thamani yake ni paundi milioni 287 kwa kipindi cha miaka 15 .
Fedha ambazo Chelsea itatengeneza kupitia mkataba huu utaifanya klabu hiyo kuwa na fedha za kutumia kwenye usajili wa wachezaji ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea fedha binafsi za mmiliki wake Roman Abramovich badala ya fedha inazotengeneza klabu yenyewe.

Mkataba huu baina ya Chelsea na Adidas ni wa tatu kusainiwa baina ya kampuni ya vifaa vya michezo na labuya England baada ya Arsenal kusaini mkataba wa paundi milioni 30 kwa mwaka na kampuni ya Puma huku Liverpool wakisaini mkataba wa paundi milioni 25 kwa mwaka na kampuni ya Warrior.