Pages

Mrisho Mpoto Kgombea Ubunge 2015

Mrisho Mpoto
MSANII nyota wa mashairi, Mrisho Mpoto “Mjomba” amsema atagombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Akiongea na kipindi cha Hot Mix cha EATV jana jioni, Mpoto alisema baadhi ya wabunge hawafanyi kazi yao ipasavyo na hivyo ameamua kuwafuata huko huko mjengoni ili akawanyooshe.

“Tumekuwa tukipiga kelele sana na tungo zetu lakini haisadii, sasa ngoja niwafuate huko huko” alisema Mpoto.
Hata hivyo Mpoto alikataa kutaja jimbo wala chama. “Kwa leo sitawaambia ni jimbo gani au chama gani, hilo ntawaambia baadae, ila ukweli ni kwamba lazima nikagombee ubunge” alisema Mpoto na kuongeza kuwa jimbo lolote linalolegalega popote pale Tanzania, linaweza kuwa ndio jimbo lake.
Mrisho alipoulizwa ataingia vipi bungeni na rasta alisema hilo atajua huko huko.