Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto
Kabwe amesema vitendo anavyofanya Spika wa Bunge havikubaliki na
anavifanya kwa makusudi ili kulinda ufisadi nchini. Zitto aliyasema hayo
katika Viwanja vya Temeke alipokuwa akihutubia Wananchi katika Mkutano
maalum wa kuwapokea Wabunge wa CHADEMA.