
Wahamiaji hao haramu wametoka katika mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma.
Kati ya hao wahamiaji haramu 5521 wamerudi nchini Rwanda, 2744 wamerejea kwao nchini Burundi na 244 warejea kwao nchini Uganda. Katika zoezi hilo siraha zipatazo 60 zimerejeshwa kwa hiari zikiwemo siraha aina ya SMG na Magobole.
Aidha, zoezi hilo la kuwarejesha wahamiaji haramu limekwenda sanjari na urejeshaji wa mali na mizigo ikiwemo jumla ya mifugo 1996 iliyorejeshwa katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda.
Serikali inapenda kusisisitiza kwamba imefurahishwa sana na ushirikiano iliyouliopata kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Uganda hasa katika kuwapokea wahamiaji hao haramu na kushirikiana na Tanzania katika zoezi hilo.
Aidha , katika zoezi hilo idadi ya wahamiaji haramu waliondoka ni kwa hiari na Serikali inawasihi wahamiaji haramu ambao bado wako nchini kuondoka haraka iwezekanavyo kabla ya hatua ya kuwaondoa kwa nguvu hazijaanza.
Zoezi la kurejea kwa wahamiaji haramu ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete, alipotoa siku 14 kwa wahamiaji kuondoka nchini kwa hiari ndani ya kipindi hicho.
Imetolewa na Idara ya Habari(MAELEZO)
No comments:
Post a Comment