Mwaka 2006 rais Jakaya Kikwete bila kulazimishwa na mtu yeyote alisema kuwa ana orodha ya wauza madawa ya kulevya nchini. Sasa ni miaka saba imepita tangu atwambie ana orodha hiyo. Wengi tunajiuliza ni kwanini imechukua muda mrefu hivyo kuwashughulikia wauza unga kama kweli ana nia au anangoja awashughulikie baada ya kustaafu? Ajabu juzi Kikwete alipodhalilishwa na Rwanda alikuwa mwepesi kuwatimua wanyarwanda waliokuwa wameishi Tanzania kwa zaidi ya miongo minne. Je Kikwete ana namna anavyonufaika na mihadarati kiasi cha siku hizi kuanza kujionyesha kama mtu anayewajali vijana kwa kukutana na mateja au kumsaidia teja Ray C. Je Kikwete anatoa picha gani kwa kuwakumbatia wauza unga huku akijifanya kuwapenda na kuwajali mateja? Je ni usanii au unafiki?
Free Thinking
No comments:
Post a Comment