Imedaiwa Daniella alifikia hatua hii baada ya paparazi huyu kuzua Ishu kuwa Nyumba ya Msanii Chameleone iliyopo huko Sseguku aliyohama na familia yake recently kwa sababu za kiusalama, ipo katika hatihati ya kutaifishwa na maafisa mkopo kutokana na Deni ambalo hawajalipa.
Taarifa hizi ambazo zimeonyesha dhahiri kumuudhi Daniella, Zilizosababisha apige mishe za kumtafuta mwandishi huyu na kuingia naye katika ugomvi mkubwa uliozaa tukio hili.
Kwa sasa Daniella anakabiliwa na kesi ya kushambulia/kupigana hadharani na yupo nje kwa dhamana ya kitita cha shilingi milioni 20 za Uganda.